Mhubiri 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mhubiri 1 (Swahili) Ecclesiastes 1 (English)

Maneno ya Mhubiri mwana wa Daudi,mfalme katika Yerusalemu. Mhubiri 1:1

The words of the Preacher, the son of David, king in Jerusalem:

Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. Mhubiri 1:2

"Vanity of vanities," says the Preacher; "Vanity of vanities, all is vanity."

Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua? Mhubiri 1:3

What does man gain from all his labor in which he labors under the sun?

Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. Mhubiri 1:4

One generation goes, and another generation comes; but the earth remains forever.

Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. Mhubiri 1:5

The sun also rises, and the sun goes down, and hurries to its place where it rises.

Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. Mhubiri 1:6

The wind goes toward the south, and turns around to the north. It turns around continually as it goes, and the wind returns again to its courses.

Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena. Mhubiri 1:7

All the rivers run into the sea, yet the sea is not full. To the place where the rivers flow, there they flow again.

Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia. Mhubiri 1:8

All things are full of weariness beyond uttering. The eye is not satisfied with seeing, nor the ear filled with hearing.

Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. Mhubiri 1:9

That which has been is that which shall be; and that which has been done is that which shall be done: and there is no new thing under the sun.

Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi. Mhubiri 1:10

Is there a thing of which it may be said, "Behold, this is new?" It has been long ago, in the ages which were before us.

Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye. Mhubiri 1:11

There is no memory of the former; neither shall there be any memory of the latter that are to come, among those that shall come after.

Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. Mhubiri 1:12

I, the Preacher, was king over Israel in Jerusalem.

Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Mhubiri 1:13

I applied my heart to seek and to search out by wisdom concerning all that is done under the sky. It is a heavy burden that God has given to the sons of men to be afflicted with.

Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo. Mhubiri 1:14

I have seen all the works that are done under the sun; and, behold, all is vanity and a chasing after wind.

Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki. Mhubiri 1:15

That which is crooked can't be made straight; and that which is lacking can't be counted.

Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa. Mhubiri 1:16

I said to myself, "Behold, I have obtained for myself great wisdom above all who were before me in Jerusalem. Yes, my heart has had great experience of wisdom and knowledge."

Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo. Mhubiri 1:17

I applied my heart to know wisdom, and to know madness and folly. I perceived that this also was a chasing after wind.

Yaani, Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni,Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko. Mhubiri 1:18

For in much wisdom is much grief; and he who increases knowledge increases sorrow.